By Martha Mboma
Migomo ya wanafunzi wa vyuo vikuu nchini imezidi kuongezeka kadri siku zinavyoenda, na migomo hiyo inayotokea katika vyuo hivi vikuu nchini inatokana na sababu mbalimbali.
Katika migomo hii ya wanafunzi wa vyuo vikuu imekuwa ikitokana na sababu mbalimbali, katika mgomo wa wanafunzi wa UDOM huu ulianzishwa na wanafunzi wa Kitivo cha sayansi na jamii ambapo walikuwa wakidai kwakutoruhusiwa kufanya mazoezi kwa vitendo, kuwa na miundo mbinu mibovu, vyakula vibovu na uhaba wa maji katika chuo chao, ndiko kulipelekea wanafunzi hao kugoma ,chuo hicho licha ya kwamba wanafunzi hao wamekuwa wakikabiliwa na matatizo mbalimbali ya kutokuwa na wahadhiri wa kutosha na wanafunzi kutopata mikopo yao katika muda muafaka na hivyo kusababisha wao kugoma na kupoteza mda mwingi wa masomo yao na baadhi ya wanafunzi wenzao kuwekwa ndani baada ya mgomo huo.
Baada ya waziri Mizengo Kayanza Peter Pinda kuongea na wahadhiri na wanafunzi wa chuo kikuu cha UDOM na kuweza kusawazisha mambo, wanafunzi hao walisitisha mgomo na kuahidiwa watatekelezewa madai yao na wahadhiri kuendelea kufundishi. Huku katika chuo kikuu Makumira kilichopo jijini Arusha mambo yalikuwa mabaya baada ya wanafunzi hao wa mwaka wa kwanza kitivo cha sheria na elimu kugoma wakidai mikopo yoa kuwa tangu novemba mwaka jana, hivyo kusababisha kuishi kwa shida na kutopata mahitaji mihimu ya kila siku. mgomo huo wa wanafunzi wa Makumira ulisababisha kufunga barabara kuu ya Arusha Moshi,kwa hali hiyo lazima watanzania tujiulize huko bodi kuna nini mbona kila kukicha mambo yanazidi kuwa mabaya.
Pia chuo kikuu kishiriki cha Tumaini Iringa wanafunzi wa kitivo cha elimu ya sanaa waligoma kutoka na kutotambulika na TCU kama kozi hii ipo katika chuo hiki na hivyo kusababisha wanafunzi hao kutopata mikopo yao. Pamoja na migomo hii inayotokea katika vyuo mbalimbali, lakini bado serikali inashindwa kutafuta mbinu mbadala ili kuepukana na tatizo hili kwa kuwa linazidi kuwasugu kadri siku zinavyozidi kwenda .
Hii ni badhi tu ,bado migomo inazidi kushika kasi hapa nchini .Hiyvo basi ikitoka kwenye vyuo vikuu muda si mrefu itahamia katika raia na serikali yao.
Hayo ndio Maisha ya Wanafunzi wa Elimu ya juu Tz.
No comments:
Post a Comment